Tohara ya kujitolea yaungwa mkono mashariki na kusini mwa Afrika

5 Disemba 2011

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS na mpango wa dharura unaohusika na ugonjwa wa ukimwi wa rais wa Marekani PEPFAR hii elo wamezindua mpango wa miaka mitano wa kuwapasha tohara wanaume kama moja ya njia ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Mpango huo uliobuiniwa na shirika la afya duniani WHO, UNAIDS, PEFPAR pamoja na benki ya dunia kwa ushirikiano na wizara za afya unataka kufanyika mara moja shughuli ya kuwapasha tohara wanaume kwenye nchi 14 mashariki na kusini mwa Afrika. Mkurugenzi wa shirika la UNAIDS Michel Sidibe amesema kuwa tohara ya wanume ni hatua katika kuhakikisha kuwepo kwa kizazi bila ugonjwa wa ukimwi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter