Mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri maisha na usalama wa chakula Sahel na Afrika Magharibi:UNEP

5 Disemba 2011

Utafiti mpya umebaini kwamba athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa upatikanaji wa rasilimali, ongezeko la idadi ya watu na uongozi dhaifu

kuwepo na ushindani mkubwa dhidi ya rasiliamali chache zilizopo na kufanya muundo wa uhamiaji kubadilika kwenye eneo la Sahel na Afrika ya Magharibi.

Utafiti huo umetoa wito wa kuwepo na uwekezaji mkubwa katika suala la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ili kupunguza hatari za kuwepo migogoro na uhamiaji wa kulazimishwa. Utafiti huo umefanywa kwa ushirikiano wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP, shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, chuo kikuu cha Umoja wa Mataifa na kamati ya kudumu ya kudhibiti ukame Sahel.

Matokeo ya utafiti huo yamewasilishwa Jumatatu kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Durban Afrika ya Kusini na hivyo kuongeza shinikizo kwa serikali kuhakikisha zinatimiza makubaliano ya kimataifa ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Utafiti huo ulijikita katika kuuangalia kiwango cha joto, mvua, ukame na mafuriko katika miaka 40 iliyopita na athari zake katika raslimali, maisha, uhamiaji na vita kwenye nchi 17 za Afrika ya Magharibi zikiwemo Chad, Mali, Mauritania, Burkina Faso, Niger, na Nigeria.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter