Skip to main content

Mchango wa watu wanaojitolea ni mkubwa sana duniani:Ban

Mchango wa watu wanaojitolea ni mkubwa sana duniani:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema duniani kote mamilioni ya watu wanaojitolea wanasaidia kuleta maendeleo endelevu na amani. Katika ujumbe maalumu wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wanaojitolea ambayo huadhimishwa kila mwaka Desemba 5 Ban amesema. Msaada wa watu hawa uko katika mifumo mbalimbali ikiwemo mashirika ya kujitolea, watu binafsi wanaojitolea katika jamii zao na huduma zitolewazo na Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kujitolea.

Ban amewapongeza mamilioni ya watu wanaojitolea na mipango ya Umoja wa Mataifa ya kujitolea kwa kuhusika na kuleta maendeleo, kutoa misaada ya kibinadamu, kulinda mazingira na kuendelea mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Naheed Haq ni naibu mratibu mtendaji wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kujitolea anasema maadhimisho ya mwaka huu ni katika kuchagiza wito wa kimataifa wa kuchukua hatua iliyotolewa mwaka 2009.

(SAUTI YA NAHEED HAQ)