Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majadiliano yanaendelea kati ya watengenezaji wa mashine za vionzi na watumizi:IAEA

Majadiliano yanaendelea kati ya watengenezaji wa mashine za vionzi na watumizi:IAEA

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA limesema mashine zaidi za mionzi katika nchi zinazoendelea ambazo ni wanachama wa shirika hilo itamaanisha wagonjwa wengi wa saratani hawatosafiri kwenda mbali iwe ndani au nje ya nchi au kusubiri kwa muda mrefu kwa ajili ya matibabu yatakayookoa maisha yao.

Shirika hilo limesema dola milioni moja zinaweza kununua computa 1626 za kutumika mashuleni, au kuruhusu watu 34 kusafiri majini kwa miezi mitatu au hata kununua magari matano ya kifahari aina ya Bentley lakini kwa wagonjwa wengi wa saratani katika nchi zinazoendelea dola milioni moja zitaleta tofauti kubwa baina ya maisha na kifo.

Huo ni ujumbe ambao IAEA umekuwa ukitoa kwa makampuni ya kutengeneza mitambo ya mionzi tangu mwaka 2009 likiyataka makampuni hayo kupunguza bei za mashine hizo kwani kwa sasa mashine na vifaa vya mionzi vinauzwa zaidi ya dola milioni 3 gharama ambayo ni kubwa sana kwa nchi masikini kumudu.Dr Shyam Shrivastava ni mwenyekiti wa AGART.

(SAUTI YA DR SHYAM SHRIVASTAVA)