Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo la UM lashutumu ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Syria.

Jopo la UM lashutumu ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Syria.

Jopo la haki la Umoja wa Mataifa hii leo limeshutumu ukiukaji wa haki za binadamu nchini Syria zikiwemo ripoti za kuteswa kwa watoto wakati serikali inapoendelea na harakati zake za kukabiliana na waandamanaji.

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayopambana na mateso imechunguza ripoti kuhusu kuendelea kuongezeka ukiukaji wa haki za binadamu nchini Syria.

Kati ya ukiukaji wa haki za binadamu uliotajwa ni pamoja za kuteswa kwa wafungwa,uvamizi kwa raia na kuuawa kwa waandamanaji wanaoandamana kwa amani na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi yao. Claudio Grossman ndiye anaongoza jopo hilo lenye wanachama kumi.

CLIP