Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washukiwa wa ugaidi wapewe haki :UM

Washukiwa wa ugaidi wapewe haki :UM

Mwongozo wa sera wa Umoja wa Mataifa unaotoa ushauri jinsi ya kufanyia mabadiliko na kuimarisha mahakama ili ziwe za haki kwa washukiwa wa ugaidi na familia zao umetolewa.

Mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayopambana na madawa ya kulevya pamoja na uhalifu Yuri Fedotov amesema kuwa haki za washukiwa zikiwemo za familia zao ni lazima zipewe kipaumbele kila wakati.

Kati ya yale yaliyopendekezwa ni pamoja na kulindwa kwa washukiwa kutoka kwenye dhuluma na kulipiza kisasi na kupewa usaidizi wa kimatibabu na kisaikolojia.