Ugonjwa wa kuendesha watangazwa nchini Djibouti

22 Novemba 2011

Wizara ya afya nchini Djibout imetangaza kutokea kwa mkurupuko wa ugonjwa wa kuendesha kwenye mji mkuu wa nchi hiyo ambapo visa 127 vya ugonjwa huo vimeripotiwa majuma mawili ya kwanza ya mwezi huu. Mwaka 2010 Djibouti iliandisha zaidi ya visa 2000 vya ugonjwa wa kuendesha.

Inaaminika kwamba ugonjwa wa kuendesha unachochewa zaidi na hali iliyo sasa kwenye pembe ya Afrika kutokana na kuwepo kwa ukame nchini Djibouti na nchi majirani hali inayoyahatarisha zaidi maisha ya watu. Kituo cha kutibu ugonjwa wa kuendeshwa kwenye hospitali kuu nchini Djibouti kina uwezo wa kutibu hadi wagonjwa 40 kwa siku. Tarik Jasarevic ni msemaji wa shirika la afya duniani WHO.

(SAUTI YA TARIK JASAREVIC)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter