Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko nchini Lebanon waharibu magari ya UM:UNIFIL

Mlipuko nchini Lebanon waharibu magari ya UM:UNIFIL

Milipuko miwili imetikisa mji wa Tyre Jumatano asubuhi nchini Lebanon na kusababisha uharibifu kwenye majengo na magari. Hadi sasa hakuna taarifa ya vifo au majeruhi. Milipuko hiyo ya mabomu imetokea kwenye mgahawa ndani ya hotel ya Queen Elissa na duka la kuuza pombe.

Wafanyakazi wengi wa mpango wa Umoja wa Mataifa Lebanon UNIFIL wanaishi kwenye mji wa Tyre. Kwa mujibu wa msemaji wa UNIFIL Andrea Tenenti serikali ya Lebanon inachunguza tukio hilo ambalo limeharibu magari mengi yakiwemo mawili ya Umoja wa Mataifa, lakini amesisitiza kwamba hakuna dalili zozote za kuonyesha kwamba shambulio hilo lilikuwa linalenga UNFIL.