Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasafirisha raia zaidi wa Sudan Kusini kwenda Kusini

IOM yasafirisha raia zaidi wa Sudan Kusini kwenda Kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linafanya mikakati ya kuwasaidia raia wa Sudan Kusini walio Kaskazini kusafiri Kusini wakitumia mashua, gari moshi na ndege ili kupunguza changamoto wanazopitia baada ya kukwama kwa meizi kadha wakingojea kusafiri Kusini.

Tarehe 14 mwezi huu msafara wa mashua 14 zikiwa na watu 300 ziliondoka mji wa Kosti ulio Kusini mwa Khartoum kuelekea Juba mji mkuu wa Sudan Kusini. Mpango huo wa IOM umefikisha idadi ya watu waliosafiri kwa kutumia mto kwenda Kusini kufikia watu 17,000 tangu kutangazwa kwa kura ya maoni ya uhuru wa Sudan Kusini. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)