Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bangladesh yapata sifa kama mshirika mkuu wa UM

Bangladesh yapata sifa kama mshirika mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon amelisifu taifa la Bangladesh akilitaja kama mshirika mkubwa katika jitihada za Umoja wa Mataifa za kulinda amani na za kimaendeleo. Ban aliyasema hayo alipokuwa akikamilisha ziara yake nchini Bangladesh.

Ban alisema kuwa aliizuru nchi ya Bangladesh kuunga mkono jitihada zilizopigwa katika kuheshimu haki za watoto na wanawake.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ban ameongeza kuwa Bangladesh iko kwenye mstari wa mbele kati kutatua changamoto za kimaendeleo.