China inaweza kufanya makubwa kukabili athari za majanga ya kimazingira:UM

9 Novemba 2011

China imeelezwa kuwa inapaswa kuchukua mstari wa mbele kabisa kuongoza dunia namna inavyotilia uzito kukabiliana na majanga ya kimazingira. Kwa mujibu wa afisa wa Umoja wa Mataifa ushirikishwaji wa sekta binafsi ili kukabiliana na mathara yatokanayo na majanga ya kimaumbile, ni hatua muhimu ambayo China inapaswa kuizingatia.

Akizungumza katika mkutano na wajasiliamali na viongozi wa biashara nchini China, Bi Margareta Wahlström,amesema kuwa bado nchi  inaweza kutoa soma kubwa kwa mataifa mengine kama itaamua kuimarisha vyanzo vyake vya kutoa unafuu baada ya kujiri kwa majanga ya kimazingira.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud