Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa usimamizi wa misitu kupanuliwa nchini Mongolia

Mradi wa usimamizi wa misitu kupanuliwa nchini Mongolia

Mradi wa kijamii ambao unatajwa kuchangia katika kumaliza ukataji haramu wa miti na moto wa misituni nchini Mongolia utapanuliwa kwenda sehemu zingine. Mradi huo ulio kwenye wilaya 15 Kaskazini mwa Mongolia umewahusisha wenyeji katika usimamizi wa ardhi yenye misitu.

Mongolia ina takriban ekari 188,000 mraba za msitu ambayo ni asilimia 12 ya ardhi yote ya nchi hiyo. Mradi huo unaungwa mkono na shirika la chakula na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na unatarajiwa kupelekwa kwenye sehemu zingine za nchi ifikapo Januari mwaka ujao.