Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia bado inakabiliwa na kipindi kigumu cha tatizo la njaa:Bowden

Somalia bado inakabiliwa na kipindi kigumu cha tatizo la njaa:Bowden

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Somalia Mark Bowden amesema taifa hilo la Pembe ya Afrika lililoghubikwa na vita bado linapitia kipindi kigumu cha njaa iliyoikumba maeneo mengi ya nchi hiyo. Ameongeza kuwa hivi sasa Somalia inakabiliwa na matatizo makubwa mawili yaliyosababishwa na vita na njaa, kwanza kumekuwa na wimbi kubwa la wakimbizi wa ndani wanaomiminika mjini Moghadishu, jambo ambalo linatoa shinikizo katika huduma na uwezo wa kuwasaidia watu hao.

Na kwa upande wa njaa Bowden amesena hivi sasa wanakimbizana na muda ili kupata msaada wa kukidhi mahitaji ya mamilioni ya watu hususani chakula katika maeneo yote yaliyoathirika. Hata hivyo amesema kuna mafanikio kiasi kikubwa yaliyopatikana hasa kwa uingiaji wa chakula cha msaada na sasa kuna mipango mipya iliyoanzishwa kama kutoa vocha za chakula na fedha na anamatumaini kuwa mwezi huu wa Novemba msaada zaidi kwa waathirika wa njaa utaingia Somalia.