Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya vitendo vya ubakaji vimefanyika wakati wa mgogoro wa Libya:ICC

Mamia ya vitendo vya ubakaji vimefanyika wakati wa mgogoro wa Libya:ICC

Mamia ya vitendo vya ubakaji vimetekelezwa wakati wa mgogoro wa Libya ambao umesababisha kuangushwa kwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi na kutangazwa ukombozi wa taifa hilo la Afrika Kaskazini. Hayo yamesemwa na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Luis Moreno Ocampo wakati akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ocampo amesema kwa sababu ubakaji unaweza kuchagiza ulipizaji kisasi na ghasia zitokanazo na kuvunjiwa hadhi nchini Libya ofisi yake sasa hivi inakusanya ushahidi bila haja ya kupata maelezo mengi ya waathirika.

(SAUTI YA LUIS MORENO OCAMPO)