Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha makubaliano ya kumaliza uhasama nchini Nepal

Ban akaribisha makubaliano ya kumaliza uhasama nchini Nepal

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya ufikiaji wa makubaliano ya amani nchini Nepal ambako pande zinazohasimiana zimefikia shabaya ya kutanzua mikwamo yao.Vyama vya kisiasa ambavyo vilishindwa kukaa meza moja, zimekubaliana kuweka shabaya ya pamoja ya utunzaji uhasama wa kisasa na zimekubaliana pia kuweka mazingira ya kukaribisha ujenzi wa katiba mpya.

Viongozi wa vyama vipatavyo vinne aidha wamekubaliana kuweka meza ya maridhiano na kuwaingiza kwenye jeshi la kitaifa askari 19,000 waliokuwa upande wa kundi la waasi wajulikanao Maoist. Akijadilia hatua hiyo, Ban amesema kuwa inatia furaha na anaikaribisha vyema na kuongeza kuwa amevutiwa na namna pande hizo zilivyokubaliana kuweka bara za la mpito la maridhiano kwa shabaya ya kumaliza kabisa mzozo wa muda mrefu.