Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanamazingira vijana kwenye maonyesho nchini Ujerumani

Wanamazingira vijana kwenye maonyesho nchini Ujerumani

Viongozi vijana wanaohusika na masuala ya kimazingira kutoka mataifa 18 yanayokua wanakusanyika nchini Ujerumani ili kuonyesha uvumbuzi wao kuhusu maendeleo. Kuanzia kubuni jiko lisilotumia makaa nchini Kenya pamoja na miradi ya watalii nchini Chile wavumbuzi hawa wanahusika na masuala ya mazingira kwenye nchi zao. Vijana hao 47 walichaguliwa kutoka kwa wengine 800 waliotuma maombi ili kuwakilisha nchi zao kwenye warsha iliyong’oa nanga kuanzia tarehe 16-na inayotarajiwa kukamilika tarehe 21 mwezi huu mjini Leverkusen nchini Ujerumani