Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa ndani wa kigeni hawatathminiwi Lebanon:UM

Wafanyakazi wa ndani wa kigeni hawatathminiwi Lebanon:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa anayefuatilia mifumo ya kisasa ya utumwa Gulnara Shahinian leo ameitaka serikali ya Lebanon kuweka sheria ya kuwalinda wafanyakazi wa nyumbani takribani 200,000 nchini humo.

Shahinian ameonya kwamba bila ulinzi wa kisheria wafanyakazi hao wataendelea kuishi katika hali mbaya ya kunyanyaswa, kuwa tegemezo kwa waajiri wao kwa kunyonywa kiuchumi, kuathirika kimwili, kisaikolojia na kunyanyaswa kimapenzi. Amesema wafanyakazi wa ndani Lebanon ambao wengi ni wageni na ni wanawake hawatambuliki kisheria. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)