Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya kuosha mikono kuadhimishwa

Siku ya kimataifa ya kuosha mikono kuadhimishwa

 

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF litajiunga na mamilioni ya watu kote duniani wakati wa siku ya kimataifa ya kuosha mikono katika kusisitiza umuhimu wa kuosha mikono kwa sabuni kama moja ya njia rahisi ya kuzuia magonjwa.

Shughuli zinatarajiwa kuandaliwa ambapo walimu, wazazi, watu mashuhuri na maafisa wa serikali watawatia moyo mamilioni ya watu katika kuzuia magonjwa hatari kama vile ugonjwa wa kuharisha. UNICEF inakadiria kuwa ugonjwa wa kuharisha unawaua watoto milioni 1.1 . Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.