Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNICEF ataka ulinzi wa haraka kwa watoto Yemen

Mkuu wa UNICEF ataka ulinzi wa haraka kwa watoto Yemen

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ametoa wito wa ulinzi wa haraka kwa watoto nchini Yemen ambao wamejikuta katika hatari ya mapigano kufuatia kuzuka machafuko mapema mwaka huu.

Bwana Anthony Lake amesema watoto hao wanapaswa kuwa mashuleni katika kipindi hiki cha mwaka lakini badala yake wanakabiliwa na watu wenye silaha badala ya waalimu, wanalengwa na risasi badala ya vitabu. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)