Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wa Rwanda kupigwa jeki

Wakulima wa Rwanda kupigwa jeki

Zaidi ya familia 125,000 ambazo zinaishi maisha ya pangu pakavu nchini Rwanda, zitapatiwa misaada ya fedha kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kilimo. Tayari Umoja wa Mataifa kupitia kitengo chake cha kusaidia wakulima wa maeneo ya vijijini, kimetenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 39.8 ambacho kinawanufaisha wakulima hao hasa lakini makundi ya wanawake na vijana wanaoendesha shughuli za kilimo katika maeneo ya vijijini.

Wakulima wa maeneo hayo hujishughulisha zaidi na kilimo cha kahawa, chai, pamoja na uzalishaji mbogo mbogo na matunda. Katika kutekeleza mpango huo Serikali y Rwanda inatazamiwa kushirikiana na IFAD na tayari wakulima 170 wameshatambuliwa na wanatazamia kuanza kutekeleza miradi yao katika awamu ya kwanza.