Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha hatua za Saudi Arabia za kuruhusu wanawake kupiga kura

Ban akaribisha hatua za Saudi Arabia za kuruhusu wanawake kupiga kura

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekaribisha hatua za mfalme wa Saudi Arabia Abdullah za kuwaruhusu wanawake kushiriki kwenye kura na kuwania nafasi kwenye miji sawa na kuwa wanachama wa Baraza la Shura.

Ban anasema kuwa anaamini kwamba hatua hii itawaakikishia haki zikiwemo za kisiasa wanawake wa Saudi Arabia. Baraza la Shura ambalo wanachama wake huchaguliwa na mfalme lina wajibu wa kuunda sheria, linahusika pia na kusimamia huduma za serikali na masuala mengine.