Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel yaidhinisha ujenzi wa makao mashariki mwa Jerusalem

Israel yaidhinisha ujenzi wa makao mashariki mwa Jerusalem

Uamuzi wa Israel wa kuidhinisha ujenzi wa makao mapya ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa Jerusalem unazorotesha kurejelewa kwa mazungumzo ya kumaliza mzozo uliopo kati ya Israel na Palestina. Hii ni kwa mujibu mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la mashariki ya kati Robert Serry.

Israel inaripotiwa kuidhinisha ujenzi wa zaidi ya nyumba 1000 mashariki mwa Jerusalem siku ya Jumanne. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky anaelezea wasi wasi uliopo kuhusu athari itakayotokana na umuzi huu kwenye mpango wa amani wa mashariki ya kati.

(SAUTI YA ROBERT SERRY)

Wale wanaotajwa kama pande nne za mashariki ya kati ni pamoja na Umoja wa Mataifa , Marekani , Jumuiya la Ulaya na Urusi.