Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya Malaria vinaweza kuokoa maisha na mapato:ITC

Vita dhidi ya Malaria vinaweza kuokoa maisha na mapato:ITC

Nchi zinazosumbuliwa na ugonjwa wa malaria zinaweza kuokoa maisha kwa kupata hasara kidogo tu kwenye mapato ya kodi, endapo wataondoa ushuru kwenye bidhaa zinaoingizwa ambazo ni muhimu kwa kupambana na gonjwa huo, umesema utafiti uliofanywa na kituo cha kimataifa cha biashara ITC.

Utafiti huo uliofanywa katika nchi 32 zinazokabiliwa na malaria Afrika, Amerika ya Kusini na Asia umebaini kwamba kuondoa ushuru kwenye madawa na kupambana na malaria, vyandara vya mbu, vifaa vya kupimia maradhi hayo na dawa za kuulia wadudu kutasaidia kupunguza gharama za kuzuia na kutibu na hivyo kusaidia mapambano ya ugonjwa huo ambao ni rahisi kuukinga.

Kwa mujibu wa ITC ingawa nchi nyingi zimeahidi kupinguza ushuru hususani barani Afrika, utafiti umeonyesha bado kodi inatozwa na mara nyingine kwa bidhaa kama vyandarua vya mbu ni ya juu sana. Utafiti huo umefanyika kwa ushirikiano na mradi wa malaria wa kupunguza kodi na ushuru M-TAP na kufadhiliwa na Bill na Melinda Gates na ushirikiano wa Roll Back Malaria.