Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi tatu zaidi zatia sahihi mkataba wa kutokuwa na uraia

Nchi tatu zaidi zatia sahihi mkataba wa kutokuwa na uraia

 

Nchi tatu zikiwemo Croatia, Nigeria na Ufilipino zimetia sahihi mkataba wa kutokuwa na uraia. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema kuwa hiyo ni hatua muhimu ya nchi kuhakikisha kuwa tatizo la ukosefu wa uraia limetatuliwa pamoja na kuzipa njia za kisheria za kuwatambua watu wasio na uraia wowote na kuwalinda.

UNHCR inakadiria kuwa karibu watu milioni 12 wanaaminika kutokuwa na uraia wa nchi yoyote kote duniani suala ambalo husababisha wao kunyimwa huduma muhimu zikiwemo za kiafya, elimu, makao na kazi.