Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kunyongwa kwa kijana nchini Iran kumelaaniwa na UM

Kunyongwa kwa kijana nchini Iran kumelaaniwa na UM

Kunyongwa kwa mvulana mmoja nchini Iran kumelaaniwa vikali na wataalamu wa huru na haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Wataalamu hao wameelezea masikitiko yao kufuatia kunyongwa kwa vijana nchini Iran licha ya wito wa kimataifa kutaka hukumu hizo zifutwe.

Kijana Alireza Molla Soltani mwenye umri wa miaka 17 alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifo mwezi uliopita kwa kosa la kumchoma kisu mwanariadha. Soltani amenyongwa hadharani siku ya Jumatano septemba 21.

Wataalamu wa huru na haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wanasema kwamba mwaka huu pekee vijana wanne wa chini ya miaka 18 wamenyongwa hadharani, na watu wengine zaidi ya 200 wamenyongwa hadharani, wengi wao wakihukumiwa kwa makosa yanayohusiana na mihadarati.

Wataalamu hao waitaka serikali ya Iran kutekeleza mara moja hatua ya kufuta hukumu ya kifo hasa kwa makosa yanayohusiana na mihadarati na kwa kesi zinazohusisha vijana wadogo.