Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umeyataka mataifa ya Asia-Pacific kuhamia kwenye Uchumi unaojali mazingira

UM umeyataka mataifa ya Asia-Pacific kuhamia kwenye Uchumi unaojali mazingira

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeyataka mataifa ya Asia na Pacific kuingia katika mapinduzi ya viwanda kwa kuzingatia uchumi unaojali mazingira ambayo yana faida kubwa katika maendeleo yatakayoinua mataifa hayo katika karne hii ya 21. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP kanda hiyo inatumia zaidi ya nusu ya rasilimali ya dunia kwa kuwa ndilo eneo lenye zaidi ya nusu ya watu wote duniani.

Ripoti inasema rasilimali zinazotumika katika kanda hiyo mfano vifaa vya ujenzi na mafuta vinavyotumika sasa vinahitaji kupungua kwa asilimia 80. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)