Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 13,000 waambukizwa kipindupindu Chad

Watu zaidi ya 13,000 waambukizwa kipindupindu Chad

Serikali ya Chad inajikongoja kukabiliana na mlipuko mkubwa wa kipindupindu ambao hadi sasa umeshawauwa watu 400 na wengine 13,000 wameambukizwa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Licha ya juhudi za serikali na mashirika ya misaada kukabiliana na mlipuko huo, ugonjwa huo unatarajiwa kuendelea kusambaa wakati huu ambao msimu wa mvua unaendelea. Sababu kubwa Umoja wa Mataifa unasema ni vifaa vya usafi.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Chad Thomas Gurtner anasema nchi hiyo ina zaidi ya watu milioni 1.5 walio na shida ya chakula na kurejea kwa Wachad wengine 80,000 kutoka Libya kunatarajiwa kufanya hali kuwa mbaya zaidi.

(SAUTI YA THOMAS GURTNER)