Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waungana na China kwenye mfuko wa fedha za kuwainua wanawake

UM waungana na China kwenye mfuko wa fedha za kuwainua wanawake

Umoja wa Mataifa umeungana na makundi kutoka China kwenye uzinduzi wa mfuko wa fedha za biashara ndogo ndogo ulio na lengo la kuwainua wanawake kwenye nchi zilizo na idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Utafiti unaonyesha kuwa moja ya vichochezi vikuu katika kuafikiwa kwa malengo ya milenia ni katika uwekezaji kwenye wanawake na wasichana kupitia masuala ya kisiasa na kiuchumi.

Naibu mratibu kwenye shirika la maendeleo la la Umoja wa Mataifa UNDP Rebeca Grynspan amesema kuwa hata kama hatua kadha zimepigwa wanawake kote duniani hawajainuka kama wanaume kwenye masuala kiuchumi, kisiasa na kijamii.