Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMO yatoa msaada kwa Tanzania baada ya ajali ya boti

IMO yatoa msaada kwa Tanzania baada ya ajali ya boti

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO leo limejitolea kusaidia serikali ya Tanzania kuchunguza chanzo cha ajali ya boti iliyotokea mwishoni mwa wiki na kuuwa watu zaidi ya 200, na kuisaidia nchi hiyo kuzuia ajali kama hiyo isitokee tena.

Efthimios E. Mitropoulos mkuu wa IMO ameelezea huzuni yake baada ya maisha ya watu wengi kupotea kwenye ajali ya boti hiyo ya spice Islander iliyotokea Jumamosi alfajiri. Na kuongeza kuwa IMO iko tayari kutoa msaada wowote wa kiufundi utakaohitajika.

Bwana Mitropolos amepongeza kazi ya kituo cha wanamaji cha Dar es salaam kwa kuratibu shughuli za uokozi, na kituo hicho kimeiambia IMO kwamba maiti 187 zimeshaopolewa na watu 619 wameokolewa.