Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watalii duniani yazidi kuongezeka:UM

Idadi ya watalii duniani yazidi kuongezeka:UM

Idadi ya watalii iliongezea kwa karibu asilimia tano kwa miezi 6 ya kwanza ya mwaka huu wakati ambapo sekta ya utalii inapoendelea kujikwamua kutoka kwenye hali mbaya ya uchumi iliyoikumba ulimwengu.

Kulingana na ripoti kutoka kwa shirika la utalii la Umoja wa mataifa UNWTO ni kuwa watalii milioni 440 walitembelea maeneo tofauti kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu ikiwa ni ongezeko la watalii milioni 19 kutoka mwaka uliopita. Maeneo yote isipokuwa kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya kati ambayo yameshuhudia ghasia tangu mwanzo wa mwaka huu yameshuhudia ongezeko la watalii mwaka huu huku asilimia kubwa ikishuhudiwa Amerika kusini, kusini mwa jangwa la sahara na kati kati pamoja na mashariki mwa bara ulaya.