Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amelaani vikali shambulio la bomu kwenye mahakama kuu ya India

Ban amelaani vikali shambulio la bomu kwenye mahakama kuu ya India

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la leo la bomu kwenye mahakama kuu ya India mjini Delhi na kuelezea matumaini yake kwamba wahusika wa shambulio hilo watafikishwa kwenye mkono wa sheria. Amerejea msimamo wake kwamba hakuna uhalali wa aina yoyote wa kufanya mashambulizi dhidi ya raia.

Kwa mujibu wa duru za habari bomu hili lilikuwa limetegwa karibu na kituo cha upekuzi nje ya mahakama mahali ambapo watu walikuwa wamepanda msururu kupata vibali vya kuingia ndani.

Watu kumi wamearifiwa kuuawa na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa kwenye shambulio hilo. Ban ameelezea mshikamano wake kwa serikali ya India na watu wa taifa hilo, pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kujeruhiwa.