Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wasafirishwa kutoka Tripoli:IOM

Wahamiaji wasafirishwa kutoka Tripoli:IOM

Wafanyakazi wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wameanza kuwapakia wahamiaji wanaotaka kuondoka mjini Tripoli Libya ili kuwapeleka Benghazi. Boti ya shirika hilo iliyozuiliwa kuuingia bandarini tangu Jumanne wiki hii hatimaye imetia nanga asubuhi ya leo baada ya hali ya usalama kuimarika bandarini hapo.

Wahamiaji hao wamekusanywa bandarini wakitokea maeneo mbalimbali ya Libya kama anavyofafanua afisa wa habari na uhusiano wa IOM Jumbe Omari Jumbe.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)