Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Somalia akutana na vingozi mjini Moghadishu

Mwakilishi wa UM Somalia akutana na vingozi mjini Moghadishu

 

Ujumbe maalum ukiongozwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Agustine Mahiga leo Jumatatu umewasili mjini Moghadishu Somalia. Kwa mujibu wa duru za habari kutoka nchini humo ujumbe wa Umoja wa mataifa umekutana na viongozi wa serikali ya mpito ya Somalia na kujadiliana kuhusu mipango ya kufanyika kwa mkutano unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya Somalia.

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika ndani ya Somalia utakuwa na lengo la kumaliza kipindi cha mpito baada ya kwa na miaka saba ya serikali za mpito.