Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makampuni binafsi yanawajibu wa kuwalinda wafanyakazi wake wa kigeni Iraq:IOM

Makampuni binafsi yanawajibu wa kuwalinda wafanyakazi wake wa kigeni Iraq:IOM

Wakati shirika la kimataifa la uhamiaji IOM likitoa msaada kwa kundi la wafanyakazi 35 wa kutoka Ukraine na Bulgaria waliotelekezwa na waajiri wao nchini Iraq, IOM imetoa wito kwa makampuni binafsi kutekeleza wajibu wao wa kuwahudumia wafanyakazi wao na kufuata sheria za kitaifa za uhamiaji, za kazi na haki za binadamu.

Wito huo umekuja wakati ambapo wafanyakazi wa IOM wanazuru sehemu mbalimbali za ujenzi kila siku ambako wahamiaji wanaishi katika hali mbaya ya kurundikana kupita kiasi, hawana huduma za taa, maeneo ni machafu yasiyo na hewa ya kutosha na bila chakula, maji na huduma za afya. Wafanyakazi hao ambao waliahidiwa ajira wa dola 2500 walipoajiriwa hadi sasa wamelipwa dola kidogo sana licha ya kufanya kazi kwa masaa mengi kwa miezi kadhaa. Jumbe Omari Jumbe afisa habari na mawasiliano wa IOM anafafanua.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)