Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi la Sudan na waasi washutumiwa kwa uhalifu wa vita Kordofan

Jeshi la Sudan na waasi washutumiwa kwa uhalifu wa vita Kordofan

Ripoti iliyotolewa leo na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kwamba ikithibitika, ukiukwaji wa sheria za kimataifa za uhalifu na sheria za kimataifa za haki za binadamu unaodiwa kufanywa kwenye jimbo la Sudan la Kordofan Kusini mwezi Juni mwaka huu huenda kawa ni uuhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Ripoti hiyo ya kurasa 12 inagusia kipindi cha Juni 5 hadi 30 ikifafanua madai ya ukiukaji mbalimbali wa sheria za kimatifa kwenye mji wa Kadugli na eneo linalozunguka milima ya Nuba ambao mapigano yalizuka Juni 5 kati ya majeshi ya serikali ya Sudan SAF na yale ya Sudan Peoples Liberation Army North (SPLA-N).

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Akifafanua zaidi kuhusu ripoti hiyo naibu kamishina wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Bi Kyung-Wha Kang, amesema hata hivyo uchunguzi zaidi unahitajika kuthibitisha madai hayo.

(SAUTI YA KYUNG-WHA KANG)