Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chombo cha kupima tsunami chafuzu jaribio la kwanza

Chombo cha kupima tsunami chafuzu jaribio la kwanza

Chombo kilichotumwa na Umoja wa Mataifa katika bahari ya Mediterranean na Atlantic kwa ajili ya kufanya utambuzi wa mapema juu ya uwezekano wa kutokea janga la tsunami, kimefaulu katika jaribio lake la kwanza.Hatua hiyo sasa inafungua milango ya kuanzishwa rasmi kwa chombo hicho kwenye eneo hilo.

Chombo hicho cha utambuzi wa mapema juu ya janga la tsunami ambacho kilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2005, kinatazamiwa kuzifaidia jumla ya nchi 31 zilizopo kwenye eneo hilo. Kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu sayansi na utamaduni UNESCO, shirika ambalo ndilo linaloratibu chombo hicho, kufaulu kwa jaribio hilo kunatoa ishara ya matumaini mapya kwa mamilioni ya watu wanaoishi kwenye eneo hilo.