Bokova alaani shambulizi kwenye kituo cha runinga Libya

8 Agosti 2011

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililotwikwa jukumu la kutetea uhuru wa vyombo vya habari amelaani shambuli lililoendeshwa na jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO kwenye kituo cha kitaifa cha runinga nchini Libya mwezi uliopita, ambapo wafanyikazi watatu waliuawa na wengine 21 kujeruhiwa. Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, Bi Irina Bokova amesema kuwa vituo vya kutoa habari havistahili kulengwa. Kwa upande wake NATO imesema kuwa shambulizi hilo liliendeshwa kuambatana na azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nambari 1973 lililoanza kutekelezwa mwezi machi linaloruhusu kuchukuliwa hatua zaidi ili kuwalinda raia nchini Libya.

Bokova alaani shambulizi kwenye kituo cha runinga Libya

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa lililotwikwa jukumu la kutetea uhuru wa vyombo vya habari amelaani shambuli lililoendeshwa na jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO kwenye kituo cha kitaifa cha runinga nchini Libya mwezi uliopita, ambapo wafanyikazi watatu waliuawa na wengine 21 kujeruhiwa. Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, Bi Irina Bokova amesema kuwa vituo vya kutoa habari havistahili kulengwa. Kwa upande wake NATO imesema kuwa shambulizi hilo liliendeshwa kuambatana na azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nambari 1973 lililoanza kutekelezwa mwezi machi linaloruhusu kuchukuliwa hatua zaidi ili kuwalinda raia nchini Libya

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud