Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asema Israel inaendelea kukiuka sheria za kimataifa

Ban asema Israel inaendelea kukiuka sheria za kimataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa amevunjwa moyo kuona Israel ikiidhinisha mpango mpya unaoruhusu kuendelea na ujenzi wa makazi katika eneo la mashariki wa Jerusalem. Chini ya mpango huo mpya, Israel inakusudia kujenga nyumba zipatazo 900 katika eneo ambalo bado linaendelea kuzua mzozo mkubwa.

Ban katika taarifa yake amesema kuwa hatua hiyo ni kuziendea kinyume sheria za kimataifa ambazo zinazoa kuendelea na shughuli zozote kwenye eneo hilo la ukanda wa Gaza. Tangu mapema mwezi septamba mwaka jana, Israel ilikataa wazo la kusitisha ujenzi huo pale ilisisitiza kutosimamisha ule mpango wa kuyaendeleza makazi hayo. Shirika la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema wakimbizi wengi waliokimbia makwao sasa wanakabiliwa na kitisho cha kuzorota kwa afya zao. Limesema kuna uwezekano wa kujitokeza matatizo kama magonwa ya utapiamlo na kwashakoo kutokana na ukosefu huo wa chakula.

Wengi wanapata chakula siyo cha kuridhisha na wengine hukosa kabisa. Ama wataalamu wa afya wanasema kuwa maeneo mengi ya Somalia watu wake wamekosa nyanjo jambo ambalo huenda likazidi kuongezeka kwa mkwamo wa kiafya.