Hali ya haki za binadamu bado mbaya nchini Iraq: UM

8 Agosti 2011

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iraq imeonya kuwa ghasia na ukiukaji wa haki za binadamu uliofichika vinaendelea kuwaathiri watu wengi nchini Iraq. Ripoti hiyo iliyotolewa hii leo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI pamoja na ofisi ya kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa iliangazia masuala kadha yakiwemo mizozo na ghasia dhidi ya raia , kuwekwa kizuizini pamoja na sheria na pia kulinda haki za makundi fulani.

Ghasia za kutumia silala zilitajwa kuwa na madhara kwa binadamu na pia huwazuia watu kupata huduma za kawaida na pia huwanyima haki zikiwemo za kukusanyika na kusema.

(SAUTI YA MAUREEN KOECH)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud