Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM aitaka Iran kutoa ushirikiano katika kushughulikia masuala ya haki za binadamu

Mtaalam wa UM aitaka Iran kutoa ushirikiano katika kushughulikia masuala ya haki za binadamu

Mtaalamu mpya wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu nchini Iran ametoa wito kwa nchi hiyo akiitaka ishirikiane naye katika kutatua masuala yaliyopendekezwa na jamii ya kimataifa.

Ahmed Shaheed amesema kuwa ana matumani kuwa utawala nchini Iran utaitambua kazi yake kama fursa ya kukabiliana na sheria za kimataifa za haki za binadamu na pia kama fursa ya kushughulikia mapendekezo ambayo yametolewa na jamii ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

SAUTI YA GEORGE  NJOGOPA)