Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya misaada ya kibanadamu inazidi kuzorota Somalia– UNHCR

Hali ya misaada ya kibanadamu inazidi kuzorota Somalia– UNHCR

Mkwamo wa kisiasa unaendelea kujiri nchini Somalia katika wakati ambapo hali ya usalama ikizidi kuzorota kunaarifiwa kuongezeka kwa makundi ya watu wanaoingia mtawanyikoni huku huduma za kibinadamu zikianguka.Kulingana na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi,makundi ya watu wameendelea kukatiza katika mji wa Mogadishu kufuatia hali mbaya ya ukosefu wa chakula ambayo pia imesababishwa na ukame.

Ongezeko hilo la watu linapindukia lile liloshuhudiwa siku chache za nyuma limesema shirika hilo la UNHCR.Shirika hilo pia linahofia uwezekano wa kuzuka kwa majanga mengine ikiwemo tatizo la utapiamlo kutokana na mkwamo huo wa ukosefu wa chakula