Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya UM vyapelekwa kwenye eneo linalozozaniwa la Abyei

Vikosi vya UM vyapelekwa kwenye eneo linalozozaniwa la Abyei

Afisa wa ngazi ya juu wa masuala ya kulinda amani kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa zaidi ya wanajeshi 500 wametumwa kwenye eneo linalozozaniwa la Abyei nchini Sudan kama mpango mpya wa Umoja wa Mataifa huku pande zinazozozana zikionyesha dalili za kutaka kusitisha makabiliano.

Hata hivyo mratibu wa masuala ya oparesheni za kulinda amani kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa changamoto zilizopo katika kushirikiana na serikali ya Sudan kuwapeleka wanajeshi kumewaacha baadhi ya wanajeshi bila chakula.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)