Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndege iliyosheheni misaada yaondoka Nairobi kwenda Mogadishu

Ndege iliyosheheni misaada yaondoka Nairobi kwenda Mogadishu

Ndege iliyosheheni misaada ya chakula imeondoka mjini Nairobi hii leo ikielekea kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo maelfu ya watu hawana chakula hasa watoto.

Somalia kwa sasa inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwai kuikumba pembe ya Afrika kwa muda wa miaka 60 iliyopita wakati zaidi ya watu 100,000 wakihamia mji wa Mogadishu kutoka maeneo yaliyotangazwa kuwa na njaa ya kusini ambapo inaripotiwa kuwa watu 2.8 wanakufa njaa. Stephanie Savariaud ni msemaji wa WFP mjini Nairobi.

(SAUTI YA STEPHANIE SAVARIAUD)