Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Myanmar kuanza kufirikia kuwaachia wafungwa wa kisiasa

Ban aitaka Myanmar kuanza kufirikia kuwaachia wafungwa wa kisiasa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya kuwepo kwa mkutano wa pamoja baina ya mshindi wa tuzo ya Nobel Aung San Suu Kyi aliyekutana na waziri wa serikali ya Myanmar na ameitaka serikali hiyo kuanza kufiria uwezekanao wa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.

Waziri anayehusika na masuala ya ustawi wa jamii U Aung Kyi,leo amekutana na mwanasiasa huyo wakijadiliana masuala mbalimbali.Ban Ki-moon amesema kuwa mkutano huo ni ishara ya wazi kwamba sasa pande hizo ziko tayari kuendeleza majadiliano ambayo mwishowe yanaweza kuleta matunda.Amesema kuwa anaamani serikali ya Myanmar itapiga hatua mbele ili kuzingatia matakwa na utashi wa wananchi wake kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa. Bi Suu Kyi aliachiwa huru mwezi Novemba mwaka jana baada ya kutumikia kifungo cha nyumbani kwa miaka 15.