Skip to main content

Ban alaani mauaji ya waziri nchini Pakistan

Ban alaani mauaji ya waziri nchini Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya waziri wa masuala ya walio wachache nchini Pakistan.

Mauaji ya Shahbaz Bhatti yamefanyika leo na alikuwa ni mpigania haki za walio wachache na mchagizaji mkubwa wa maingiliano ya kidini nchini humo. Mauaji ya Bhatti yanafuatia yale ya gavana wa Punjab mwezi Januari mwaka huu ambayo Katibu Mkuu aliyalaani vikali pia.

Ban ameichagiza serikali ya Pakistan kuendelea na juhudi za kupambana na ugaidi, kulinda haki za wachache na kuvumiliana. Pia ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya bwana Bhatti, serikali na watu wa Pakistan.