Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya chakula yawafikia waliothirika na njaa nchini Somalia

Misaada ya chakula yawafikia waliothirika na njaa nchini Somalia

Karibu watu milioni 1.5 wanaendelea kupokea chakula cha dharura kila siku nchini Somalia hata baada ya madai ya kundi la wanamgambo la Al Shabbab kuwa wanazuia usafiri kwenye sehemu nyingi za nchi. Mashirika ya kutoa misaada ya Umoja wa Mataifa yana mipango ya kupeleka misaada eneo la Kusini mwa Somalia ambapo watu milioni 2.8 wanakabiliwa na njaa.

Mkurugenzi wa wa shirika la mpango wa chakula duniani FAO Josette Sheeran anasema kuwa misaada inawafikia wanaoihitaji na kuongeza kuwa si sehemu zote zinazofikika nchini Somalia. Mratibu wa masuala ya dharura kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos anasema kuwa hali mbaya ya usalama haiwezi kuzuia jitihada za kutoa misaada kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi.