Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji wa chakula kuanza kwenda nchini Somalia

Usafirishaji wa chakula kuanza kwenda nchini Somalia

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP litaanzisha shughuli ya kusafirisha misaada kwenda nchini Somalia baada ya nchi hiyo kukumbwa na ukame ambao hujawai kushuhudiwa kwa muda wa miaka 60 iliyopita.Hali ya njaa imetangazwa kwenye sehemu mbili Kusini mwa nchi ambapo mashirika ya kutoa misaada hayafiki.

Misaada ya kwanza itapelekwa kwenye mji mkuu Mogadishu kuwasaidia maelfu ya watu ambao hawana chakula. Inakadiriwa kuwa watu milioni 12 wameathiriwa pakubwa na ukame kwenye pembe ya Afrika huku Somalia ikiathirika zaidi. Emilia Casella ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA EMILIA CASELLA)