Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi wanaokimbia njaa waingia mjini Mogadishu

Watu zaidi wanaokimbia njaa waingia mjini Mogadishu

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Matiafa UNHCR linasema kuwa kila siku takriban watu 1000 wanawasili mjini Mogadishu baada ya kukimbia maeneo yanayokumbwa na njaa Kusini mwa Somalia. Msemaji wa UNHCR mjini Geneva Melissa Fleming anasema kuwa maelfu ya wengine wanachukua uamuzi hatari kwa kuhama nchi yao.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)

Kwenye kambi ya Daadab nchini Kenya karibu wakimbizi 1500 kutoka Somalia wanawasili kila siku. Kenya imeshuhudia wakimbizi 100,000 wapya mwaka huu pekee huku Ethiopia ikipokea wakimbizi 78,000. Emmanuel Nyabera ni msemaji wa UNHCR nchini Kenya.

(SAUTI YA EMMANUEL NYABERA)