Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka kuwepo kwa umakini wakati wa ufungwaji wa kambi Haiti

UM wataka kuwepo kwa umakini wakati wa ufungwaji wa kambi Haiti

Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakati huu ambapo Haiti ikiwa kwenye mchato wa kuyafunga makambi yaliyowahifadhia wananchi walioathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi la mwaka uliopita, lazima shughuli hiyo ifanywe kwa uangalifu na umakini .Katika taarifa yake juu ya hatua hiyo,Ofisi ya Kamishna ya haki za binadamu umesema kuwa jambo linalopaswa kuzingatiwa ni kuhakikisha hakuna raia wanaangukia kwenye shida ya kupata makazi.

Mamlaka ya Haiti mwishoni mwa wiki ilitangaza kuanza kuyafunga makambi yote ambayo yalitumika kuhifadhia zaidi ya familia 400 zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi.Umoja huo wa Mataifa umesisitiza kuwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa sasa za kuanza kulijenga upya taifa hilo lazima zizingatie makundi yote hasa kwenye maeneo ya upatikanaji wa makazi ya uhakika.