Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lataka kundi la LRA kuweka silaha chini

Baraza la Usalama lataka kundi la LRA kuweka silaha chini

Baraza la Usalama leo limelaani vikali matukio ya mashambulizi yanayoendelea kufanywa na vikosi vya Lord resistance army LRA huko Afrika ya Kati na kulitaka kundi hilo kusitisha mara moja vitendo hivyo.Mashambulizi hayo yasiyo na macho yamesababisha mamia kwa maeflu ya wananchi kuingia kwenye mtawanyiko. Ripoti zinasema kuwa zaidi ya watu 380,000 wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na mashambulizi hayo.

Katika taarifa yake baraza hilo la usalama limeelezea masikitiko yake namna mashambulizi hayo kwa raia wasio na hatia na kutaka ukomeshwaji.Imewataka wanamgambo hao kusitisha kuweka silaha chini ili kujenga mustakabala mpya wenye mafungamano mema kwa wananchi.